Paparazzi Athumani Hamis kuanza kampeni Maalum ya Usalama BarabaraniNaibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Silima  akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kumtangaza  Athuman Hamisi (kulia) kuwa Balozi wa Usalama Barabarani kitaifa.

Athumani Hamisi anataraji kuanza kampeni maalum ya kuhamasisha jamii juu ya matumizi sahihi ya vyombo vya usafiri kwa kufanya kampeni hiyo kuanzia mwezi Desemba ambao umeelezwa kuwa na matukio mengi ya ajali na kusababisha vifo na ulemavu.

Pia wito umetolewa kwa wadau mbalimbali nchini na nje ya nchi ambao watapenda kusaidia jitihada hizo za Athumani Hamisi kuchangia ama moja kwa moja kwake au kupitia Kamati ya Kitaifa ya Usalama Barabarani ambayo Mwenyekiti wake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nadani, Pereira Silima  na Katibu ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna wa Polisi, Mohamed Mpinga.  
Athumani ni Mwandishi wa habari wa shirika la Magazeti ya Serikali, Tanzania Standard Newspapers (TSN), inayochapisha magazeti ya Daily News na Habari Leo na alipata ajali ya gari huko Rufiji takribani miaka mitano iliyopita hali iliyompelekea ulemavu ambapo viungo vya mwili wake vimepooza.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List