Imeelezwa
wanasiasa wengi nchini wanaweza kupata na maradhi ya vidonda vya tumbo, mara
baada ya uchaguzi mkuu wa Raisi,wabunge na madiwani utakao fanyika oktoba mwaka
huu
Hayo
yameelezwa na kituo cha utafiti na matibabu ya Tumbo nchini ,TABCCOM, ambacho
kimesema wanasiasa wanaokabiliwa na tatizo hilo ni wale watakao shindwa katika
uchaguzi huo mkuu
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar Es
Salaam ,Mkurugenzi wa TABCCOM ,Dokta Khalid Hassein Mbwenya ,amesema kuna
makundi matatu yanayokabiliwa na maradhi ya Vidonda vya Tumbo lakini wanasiasa
ndilo kundi linalokabiliwa na tatizo hilo kuliko makundi mengine.
Amesema
makundi mengine yanayokabiliwa na tatizo hilo ni wafanyakazi na
wafanyabiashara,kutokana na kutumia muda mwingi wa kufanya shughu;I zao na
kupitiliza muda wa kula,lakini wanasiaa wana hatari zaidi kutokana na msongo wa
mawazo na kutokula.
Utafiti wa
tiba hiyo umefanyika katika nchi za Tanzania,Burundi,Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo,Camoro na Msumbiji.
0 comments:
Chapisha Maoni