TAIFA LA TANZANIA LIMEMPOTEZA MPAMBANAJI DHIDI YA UFISADI MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA

Mchungaji Christopher Mtikila mwanasiasa mkongwe na ambaye amepata umaarufu zaidi kutokana na mapambano dhidi ya maadili na vita dhidi ufisadi amefariki leo Dunia.Chanzo cha kifo chake inasemekana kuwa ni ajali ya Gari iliyotokea Chalinze maeneo ya Msolwa.
Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa ni mmoja wa wagombea urais wa Tanzania lakini kutokana na baadhi ya sababu alishindwa kufikia vigezo vya kugombea baada ya mgombea mwenza kuchelewa kufika wakati wa urudishaji wa fomu.

Mchungaji Christopher Mtikila nyakati za mwisho wa uhai wake alitangaza kusaidia wananchi wa Tanzania kipindi hiki cha uchaguzi kwa kupinga Ufisadi hususani kwa wagombea wa Urais.Mchungaji Christopher Mtikila alisema Fisadi Papa hawezi kuwa na uhalali wa kugombea Urais na kupata Uraisi hivyo Lowassa hana uhalali wa kuwa Rais wa Tanzania.

Mchungaji Christopher Mtikila alikuwa ni mwana siasa mwenye uwezo wa pekee na maarufu kwa kushindana na kushinda kesi zake mahakamani pamoja na kupinga waziwazi Ufisadi bila uoga.

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani amethibisha kutokea kwa ajali hiyo na wanaendelea na uchunguzi lakini mpaka sasa wanamshikilia Dereva wa gari hilo.





    Mchungaji Christopher Mtikila enzi za uhai wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List