Rais mstaafu wa awamu ya pill, Ally Hassan Mwinyi amezindua kiwanda cha kuzalisha zana za Kilomo na ujenzi zitakazokuwa zinauzwa nchini.
Kiwanda hicho cha AVIC-SHANTUI Tanzania limited kitakachomilikiwa na Wachina na kinatalajiwa kuzalisha bidhaa zake kwa kutumia chuma toka Tanzania hivyo kukuza Uchumi wa Tanzania.
Rais Mstaafu Ally Hassan Mwinyi amewataka Wananchi kutumia firsa hii Katika kuboresha Kilomo na kukuza biashara.
Naye katibu Mkuu wizara ya biashara na Viwanda Uledi Mussa amewapongeza umoja wa kampuni hizo mbili kutoka China kwa kuwezesha Tanzania kupata kiwanda hicho.
Mkurugenzi Mkuu EPZA eneo maalum la uwekezaji na mauzo ya nje, Joseph Simbakalia amesema jamii yenye Amani ina fursa kubwa ya maendeleo.
Tanzania inatarajia kunufaika na kiwanda hicho cha AVIC-SHANTUI Tanzania limited kinachotarajiwa kuuza bidhaa za Kilomo na ujenzi.
0 comments:
Chapisha Maoni