VYUO VIKUU VYASHAURIWA KUHESHIMU SHERIA INAYOLINDA HAKI ZA WAANDISHI

Vyuo vikuu vyashauriwa  kuheshimu sheria iliyopitishwa 2014,kanuni hiyo iliyopitishwa na serikali ya kutakiwa kulipia Leseni za kudurufu kazi za maandishi kwa mujibu wa sheria iliyosainiwa mwaka 2014 na Waziri wa Viwanda na Biashara.

Kupitishwa kwa sheria hiyo kunalenga kulinda na kutetea kazi mbalimbali za waandishi wa Vitabu na Makala mbalimbali.Praxeda Kimath Mwanasheria na Afisa Leseni wa Taasisi ya kusimamia na kulinda haki za kudurufu waandishi na machapisho Tanzania(KOPITAN) amesema jumla ya Vyuo vikuu vilivyopo nchini ni 32 lakini bado kuna tatizo la uelewa kuhusu umuhimu wa kulipia leseni hizo ambapo tangu sheria hiyo isainiwe ni Vyuo vikuu viwili tu mpaka sasa vilivyolipia haki ya kudurufu na kupatiwa leseni.

Kimath ameiomba Serikali kuwasaidia kuongeza juhudi za kuelimisha vyuo vikuu nchini ili waweze kulipia leseni zao na kufanikisha mkakati wa kudhibiti kazi za waandishi wa vitabu na makala zisitumike vibaya.






Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List