Wakazi wa Temeke walalamikia tatizo la mrundikano wa Takataka katika maeneo ya Makazi.

Wakazi wa manispaa ya Temeke wamelalamikia  Uongozi wa manispaa hiyo kwa kuacha Mrundikano mkubwa wa uchafu katika maeneo mbalimbali hivyo kupata wasiwasi wa kupata magonjwa ya mlipuko kama Kipindupindu.Afisa mtendaji wa mtaa huo amesema yeye sio muongeaji rasmi kwasababu si eneo lake la kazi na eneo hilo limekuwa la mda mrefu Tangu ameajiliwa katika ofisi hiyo.

Ally Khatibu mkuu wa idara ya Usafi wa mazingira Manispaa ya Temeke amekili kuwa eneo hilo sio rasmi kwa kumwaga taka bali ni kizimba kwa kuweka taka kwa muda ila kutokana na wingi wa kata kutupa taka zake katika eneo hilo kumsababisha tatizo hilo.Pia amewaomba wananchiwashirikiane kwa pamoja katika usafi wa Mazingira,Kwani wameomba fedha katika bajeti ya 2015 na 2016 kwa ajili ya kuanzisha dampo la kisasa katika eneo la kisalawe.

Tatizo la mrundikano wa taka katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya temeke yamekuwa kero kwa wakazi wa maeneo hayo huku viongozi wa serikali wakibaki kimya.

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List