Aliyekuwa waziri mkuu nchini Tanzania na mwanachama wa Chama cha Chadema Edward Lowassa, amehojiwa na kuondoka katika afisi ya mkurugenzi wa uchunguzi wa jinai baada ya kutakiwa kufika katika afisi hiyo siku ya Jumatatu kwa sababu zisizojulikana .
Kulingana na gazeti la The Citizen, Bwana Lowassa ambaye alitakiwa kuwasili katika afisi ya DCIO muda wa saa nne aliwasili saa tatu na dakika 58 asubuhi.
Msafara wake ulikuwa na magari sita ikiwemo magari mawaili ya polisi yaliokuwa na polisi waliojihami.
The Citizen linasema kuwa usalama ulikuwa umeimarishwa katika barabara ya Ohio.
Waandishi habari walikatazwa kuchukua picha za bwana Lowassa.
Katika mahojiano ya simu na gazeti la The Citizen, alisema kuwa anashuku kwamba agizo hilo la kutakiwa kujiwasilisha linatokana na matamshi aliyotoa mjini Dar es salaam siku ya Ijumaa wakati wa hotuba ya Iftar.
Wakati wa hotuba hiyo, alimtaka rais Magufuli kuwaachilia huru wahubiri wa Kiislamu ambao walikuwa wamekamatwa kwa zaidi ya miaka minne bila kesi zao kuamuliwa.
TUME YA TOA KIBALI KWA ASASI 256 KUFANYA KAZI WAKATI WA UCHAGUZI MKUU 2025
-
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetoa vibali vya kutoa elimu ya
mpiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa t...
Saa 20 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni