Jumanne, 9 Septemba 2014

WEZI WA PEMBEJEO MWISHO TANZANIA,amesema WAZIRI WA KILIMO ENG.CHRISTOPHER CHIZZA

Serikali imejipanga kuondoa tatizo la wizi wa pembejeo ambalo linadaiwa kuwasumbua  wakulima wadogo wadogo kwa muda mrefu kutokana na kudhurumiwa pembejeo na baadhi ya Watendaji wa serikali wasio waaminifu .

Waziri wa kilimo Eng . Christopher Chizza amesema kwa sasa serikali imebuni taratibu mpya  zitakazokuwa zikisimamiwa na wakulima wenyewe kupitia vikundi vidogo vidogo vilivyoundwa kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo .

Kupitia taarifa yake kwa wakulima hao Waziri Chizza anawataka wakulima kutovunjika moyo kutokana na serikali kubuni mbinu mpya za kudhibiti tatizo hilo ambapo pia itawanufanisha wakulima hao wadogo kiuchumi

Kwa sasa anawataka wakulima hao kujipanga upya kupitia vikundi  vyao ambavyo vitawasiidia kupata mikopo katika tasisi za mikopo na kurudisha kwa riba ndogo iliyo punguzwa kwa asilimia 4 kupitia serikalini.

Kilimo cha hapa nchini kimeendelea kutawaliwa na wakulima wadogo wadogo ambapo karibu asilimia 70 ya kilimo hicho kinategemea jembe la mkono,asilimia 20 jembe la kukokotwa na ng'ombe na asilimia 10 matumizi ya trekta.

Eng:Christopher Chizza(Waziri wa Kilimo)

Baadhi ya mazao yanayozalishwa Tanzania na wakulima wa Ndani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni