Alhamisi, 30 Aprili 2015

MBUNGE WA BAHI ASHINDA KESI YA KUOMBA RUSHWA

Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma kwa tiketi ya CCM, Omary Badwel, aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga ameachiliwa huru na Hakimu Mkazi Kisutu Hellen Riwa, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa huyo.
Hakimu huyo alisema “katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haioneshi wazi kwamba mbunge huyo aliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha.”
"Kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuithibitishia mahakama pasipo shaka kwamba mbunge huyo ametenda makosa hayo, mshtakiwa upo huru kuanzia sasa. HAta hivyo napenda kukuasa kuwa kama una tofauti na watu katika jimbo lako kuwa makini na ujihadhari pamoja na kujirekebisha kama una tabia ya kuombaomba jirekebishe na kuepuka kugusa vitu vya watu," alisema hakimu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni