Alhamisi, 29 Juni 2017

AVEVA NA KABURU WARUDISHWA MAHABUSU

Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' wamerudishwa rumande mpaka July 13, 2017.
Mheshimiwa Hakimu Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya jijini Dar Es Salaam alisema kuwa makosa yao matatu kati ya matano yanayowakabili hayana dhamana kwani yanahusiana na kughushi. Kwa misingi hiyo ya kisheria, Hakimu aliamua watuhumiwa hao waende rumande hadi tarehe 13 Julai kesi hiyo itakapotajwa tena.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni