TANZIA :
BURIANI BRADLEY, VITA UMEIPIGA
Mtoto Bradley Lowery (6), ambaye amekuwa anateseka kwa ugonjwa wa kansa aina ya neuroblastoma ambao ni nadra tangu akiwa na umri wa miaka miwili, amefariki dunia.
Bradley alifahamika kwa mapenzi yake ya soka na alikuwa akiishabikia sana timu Sunderland na alikuwa rafiki wa karibu sana wa mchezaji Jermaine Bradley.
Familia yake imethibitisha taarifa hii kwa kutoa ujumbe ulisema "Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo.
"Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine. Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunish
wa na kifo chake."
Kutoka SDM production media tunaungana na wapenda soka duniani kumwomba Mungu kuipumzisha roho ya Bradley Lowrey mahali pema peponi."
DKT. YONAZI TUKO TAYARI KWA CHAN 2025
-
Dkt. Jim Yonazi aongoza makatibu kukagua viwanja,asema sasa Tanzania
timamu kwa CHAN .
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt....
Saa 18 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni