Rais Jose Mujica amesema maafisa wa FIFA wamuadhibu Suarez kwa unyonge wake
Rais wa Uruguay Jose Mujica amewatukana maafisa wa FIFA kwa kuwaita ''kundi la watoto wa Mbwa'' au "a bunch of old sons of bitches".
Hii ni baada ya maafisa wa shirikisho hilo kumpiga marufuku mchezaji wa nchi hiyo Luis Suarez.
Suarez alipata adhabu hiyo ambayo inasemekana kuwa kali sana kuwahi kutolewa katika hoistoria ya kombe la dunia kwa kumuua mchezaji wa Italia Giorgio Chiellini.Mchezaji huyo aliitaja adhabu hiyo ya marufuku ya miezi minne ikiwemo kutocheza mechi 19 za kimataifa kama adhabu ya kinazi.
Rais Mujica anasifika kwa kutotafuna maneo yake pamoja na ukali wa matamshi yake.
Aliyatoa matamshi yake kupitia televishini ya taifa alipokuwa anawapokea wachezaji wa timu hiyo baada ya kutolewa nje ya michuano ya kombe la dunia katika awamu ya kumi na sita bora.
Rais huyo alifunika mdomo wake kwa mshutuko wa kile alichosema , lakini wandishi wa habari tayari walikuwa wamemrekodi.Pia aliwaambia kuyachapisha matamshi yake alipohojiwa ikiwa alitaka kujirekebisha.
Rais huyo alisema kuwa FIFA ilimuadhibu Suarez kwa sababu ya maisha yake ya zamani ambayo yalikuwa ya unyonge.
Pia alitaja adhabu hiyo kama aibu kubwa sana kwa historia ya FIFA.
About Unknown
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Chapisha Maoni