BABA NABII PAULO BENDELA AKIWA KATIKA KAZI YA UTUMISHI WA MUNGU AMEWAUNGANISHA WANANDOA WALIOACHANA ZAIDI MIAKA 22 SASA WARUDI KATIKA NDOA YAO

Baba Bendala amesema ukimtumikia na kumwamini Yesu kristo kila jambo linawezekana huku akiwataka Wanadamu wamtumikie Mwenyezi Mungu. amesema  wamtumikie MUNGU na baraka katika Nyumba zao zitakuwepo daima, familia itakuwa bora, watoto watapata malezi ya Baba na Mama nyumba zao zitakuwa na Imani, Upendo, na maadili  mema ya kiroho Kutokana na uwepo wa hofu ya Mungu katika  familia hizo. 


BI Christina Elias Masoud ambaye aliachana na Mume wake Bwana Self Binas Mkubiru baada ya kuongeza Mke wa Pili ndoa hiyo ya mama huyo  ilikuwa ni matatizo na hatimaye waliweza kuachana alipewa taraka na hatimaye aliondoka na Watoto wake Watatu na kurudi Kijijini Kibiti Rufiji. Maisha yalikuwa magumu yeye na Watoto kupata haki zao za Msingi na amewalea katika Mazingira magumu hadi wamefika nao wakati wa kujitegemea. Mama huyo aliamua kwenda kwenye Ibada ya Maombezi  katika Kanisa la Ufunuo Sinza. Baba Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufunuo Tanzania Paulo Bendera alimgusa akamwambia umekuwa ukiwa na mawazo ya kutaka kurudi katika ndoa yako umeachika  zaidi ya miaka 22 sasa lakini nakuhakikishia kwa Mungu akuna kinachoshindikana. Mpigie Simu Mume wako mwambie unahitajika na Baba Nabii Bendera  aje asikie Sauti yenye nguvu  ya Bwana Yesu Kristo naye atakubali. Bwana Self Binas Mkubiru amerudiana na Mke  wake ambaye waliachana zaidi ya miaka 22 iliyopita Baba Nabii Bendera ameweza kurudisha upya ndoa iliyovunjika.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List