MSANII Snura ametoa wimbo wake mpya
unaokwenda kwa jina la ‘Nimevurugwa’.Wimbo huo utakuwa ni wa pili ambapo awali
aliachia wimbo wa ‘Majanga’ ambao bado
unafanya vema katika tasnia ya muziki katika matamasha mbalimbali na hafla anazoalikwa.
Wimbo huo ambao ameupiga katika miondoko ya
mduara umetambulishwa jana katika vituo mbalimbali vya redio.
Baadhi ya wadau wa muziki waliopata fursa ya kuusikiliza wameupa sifa wimbo
huo ambao unazungumzia mambo kadha wa kadha
katika jamii, elimu na maisha kwa ujumla.
Awali msanii huyo ambaye nyota yake ilianza kung’ara katika uchezaji wa filamu lakini baadaye aligeukia muziki.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Chapisha Maoni