Shafii Dauda aliyeshindwa kurejesha fomu ya uchaguzi wa Taswa |
JUMLA ya waombaji 27 kati ya 28 wamerejesha
fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya
ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA)
utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu
hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.
Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni
Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga,
Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest
Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard
Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.
Mhazini Msaidizi ni Elius John
Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na
Mohamed Salim Mkangara.
Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas
Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Patrick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir
Ally Mhando pekee.
Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti
ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga.
Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas
Pinto.
Mgombea mwingine wa nafasi hiyo, Shaffih Kajuna Dauda hakurudisha fomu kwa madai ya kubanwa na moja ya vipengele vya katiba ya chama hicho na yeye ameonyesha kuridhika kujiweka kando bila kinyongo.
0 comments:
Chapisha Maoni