Mkurugenzi wa ANSAF, Audax Rukonge alipokuwa akieleza maudhui ya siku ya Mwaka wa Kilimo wa Afrika |
Ukaguzi wa shamba la mfano katika kijiji cha Kaning'ombe ulifanywa |
Wasanii, Mrisho Mpoto na Profesa J ambao ni mabalozi wa kampeni ya "Kilimo Kinalipa, Jikite" walikuwepo |
Naye Mwakilishi wa shirika la Afrika One kutoka Afrika Kusini alikuwepo kuelezea kilimo kinavyoweza kuwatoa watanzania |
Msanii Dokii naye alisema mambo na jinsi kilimo kinavyomtoa |
Wazee wa kampeni, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walisema maneno yao kwa kupokezana wakieleza jinsi kilimo kinavyoweza kuwa mkombozi kama dhamira itakuwepo |
Mkulima wa mfano, Eusebio Mbagile alizungumzia changamoto wanazopata wakulima wadogo katika shughuli hiyo ya kilimo |
Baada ya kueleza changamoto zinazowakabili, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk Christine Ishengoma aliishia kwa kupata ka KUKU ka zawadi ili akale yeye na familia yake |
JUKWAA
la Wadau wa Kilimo (ANSAF) limekumbushia ahadi ya kutenga asilimia 10 ya bajeti ya nchi kwa
ajili ya Kilimo, iliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2012.
Mkurugenzi
wa ANSAF, Audax Rukonge aliyasema hayo leo wakati Makamu wa Rais, Dk Mohamed
Gharib Bilal aliyewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christine Ishengoma
akizindua Mwaka wa Kilimo wa Afrika.
Uzinduzi
wa mwaka huo unaokwenda na kampeni iliyopewa jina la ‘Kilimo Kinalipa, Jikite’
ilifanyika katika kijiji cha Kaning;ombe, wilayani Iringa mkoani Iringa.
Mbali
na ANSAF, wengine wanaoratibu kampeni hiyo ni mashirika ya Cloud Media na Afrika
ONE inayowataka viongozi wa Afrika kutimiza Azimio la Maputo linalohimiza
uwekezaji katika kilimo
Mabalozi
wa kampeni hiyo, wasanii maarufu, Mrisho Mpoto, Profesa J na Masoud Kipanya walizungumzia
namna kilimo kinavyoweza kuwakwamua vijana na lindi la umasikini huku msanii wa
filamu nchini Dokii akieleza mafanikio yake ya kilimo katika shamba lake
lililoko wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Mkurugenzi
wa ANSAF, alisema kwa kupitia azimio hilo la Maputo wakuu wa nchi walikubalina
watenge bajeti ya asilimia 10 ya bajeti zao kwa ajili ya kilimo.
Alisema
kiwango hicho kilitarajiwa kutosha kuchangia kuongeza uzalishaji na tija,
kukuza sekta ya kilimo kwa asilimia 6 kwa mwaka na kuondoa tatizo la njaa na
umasikini.
“Leo
hii ni miaka 10 tangu makubaliano ya Maputo. Ni nchi nane tu za Afrika
zimetimiza ahadi hiyo; Tanzania haimo katika nchi hizo,” alisema bila kuzitaja.
Alisema
tafiti zinathibitisha kuwa kilimo huchangia mara 11 zaidi katika kuondoa
umasikini ikilinganishwa na uwekezaji mwingine.
Alisema
kama taifa limedhamiria kuondoa umasikini ni lazima kukipatia kilimo mtazamo
mpya wa kiuchumi, usiokuwa na chembe za kisiasa huku uwekezaji ukifanywa kwenye
maeneo ya kimkakati.
Katika
hotuba yake kwa wadau wa Kilimo, Makamu wa Rais alisema kilimo ni lazima
kiendelezwe kwa usalama wa chakula na maisha.
Alisema
program ya kuendeleza kilimo ilizinduliwa mwaka 2005/2006 ikilenga kilimo kikue
kwa asilimia sita kutoka asilimia nne ya hivisasa.
Alisema
kwa kushirikisha sekta binafsi program hiyo inalenga pia kuwatoa wakulima
katika kilimo cha kujikimu ili kiwe cha kibiashara.
“Tunatakiwa
kuwa na muda maalumu wa kushughulikia ahadi ya Maputo ya kutenga asilimia 10 ya
bajeti ya serikali, kufanya mabiliko ya sera na kuongeza uwajibikaji katika
sekta hiyo,” alisema.
Mmoja
wa wakulima wa mfano katika kijiji hicho, Eusebio Mbangile alisema shughuli ya
kilimo ni kero kubwa kwa wakulima wadogo kutokana na ukubwa wa bei za pembejeo,
upatikanaji wake na masoko.
Alisema
“ninazo heka 45; ninazolima ni 19, wakati wa masika 15 na wakati wa kiangazi
heka nne, kwa wastani natumia karibu Sh Milioni 4 kwa shughuli nzima ya kilimo
kila mwaka;” alisema huku akionesha mashamba yake hayo ya mahindi.
Alisema
kwa wastani hupata gunia 25 za mahindi kwa kila heka ambayo hata hivyo huwa
hauzi kwa vipimo vinavyokubalika kisheria.
Alisema
walanguzi wamekuwa wakinunua gunia la mahindi lenye ujazo wa kilo 150 hadi 160
kwa Sh 38,000 tu hali inayowapa hasara kubwa na kuwafanya waendelee kuwa
masikini.
0 comments:
Chapisha Maoni