BENDI mpya wa muziki wa dansi ya Ruvu Stars, inatarajiwa kutua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao tatu mpya.
Mmoja wa viongozi na muimbaji wa bendi hiyo yenye maskani yake Mlandizi, Pwani Rogert Hegga 'Catapillar', alisema wataingia studio kuanzia leo kwa ajili ya kurekodi nyimbo hizo za kuwatambulisha.
Hegga alizitaja nyimbo kuwa ni pamoja na 'Network Love' utunzi wa Mhina Panduka 'Baba Danny' a.k.a Toto Tundu, 'Jua Kali' wa Kuziwa Kalala na 'Spirit' ambao ni utunzi wake (Hegga).
"Tunatarajia kutua jiji kesho kwa ajili ya kuja kuingia studio kurekodi nyimbo zetu tatu mpya ambazo ndizo zitakazotutambulisha kwa mashabiki," alisema Hegga.
Mtunzi na muimbaji huyo wa zamani wa bendi kadhaa maarufu nchini ikiwamo ya African Stars, Mchinga Sound, G8 Wana Timbatimba na Extra Bongo, alisema mashabiki wasubiri kupata uhondo kwao baada ya kumalizika kwa kazi hiyo yua kurekodi.
"Mashabiki wajiandae tu kupata burudani, nyimbo hizi zitaleta mapinduzi makubwa katika muziki wa dansi kwani zimeenda shule na studio tunayorekodia itazidisha manjonjo zaidi," alisema.
Alipoulizwa jina la studio hiyo, Hegga alisema wasingependa kuweka hadharani kwa sasa mpaka wakimaliza kurekodi.
Rogert Hegga |

0 comments:
Chapisha Maoni