Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es Salaam. |
Picha na Hassan Silayo
******************************************
Frank Mvungi
Serikali
ya Tanzania imesema haina ugomvi na nchi jirani kwa kuwa ni wadau wa
maendeleo katika kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa zilizopo.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh.
Bernard Membe wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es
salaam kuhusu taarifa mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari
kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda.
Akieleza
zaidi Mh.Membe alisema vyombo vya habari vinalojukumu kubwa la
kuielimisha jamii na kuimarisha uhusiano kati Tanzania na nchi jirani na
si kufanya jambo lolote linaloweza kuleta tofauti kati ya Taifa moja na
jingine.
Mh.
Membe amesema kuwa Tanzania ni nchi inayotumia njia za Kidiplomasia
kuondoa tofauti zozote zitakazojitokeza kati yake na nchi yoyote na
haina mpango wa kuingia kwenye mgogoro na nchi yoyote ile.
Aliongeza
kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa kisiwa cha amani na mfano bora
katika bara la Afrika ndio maana imekuwa mstari wa mbele katika kutatua
migogoro ndani ya bara la Afrika.
Akifafanua
zaidi Mh. Membe amesema Tanzania imepeleka vikosi vyake Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo,Lebanon,Sudan ya Kusini, katika kutimiza jukumu la
kulinda amani Duniani.
“Tunafikri
ni vyema Jukumu la ulinzi wa Bara la Afrika likawa mikononi mwa Afrika
yenyewe” alisisitiza Mh.Membe alipokuwa akifafanua kuhusu nafasi ya
Tanzania katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya
Bara la Afrika.
Pia
alieleza kuwa tangu harakati za ukombozi wa bara la Afrika Tanzania
imekuwa makao makuu ya vyama vyote vya ukombozi barani Afrika na
kusaidia katika harakati za kuleta ukombozi .
Serikali
ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
mwaka huu imepanga kufanya maandalizi mazuri yatakayoiwezesha timu ya
Taifa kushiriki na kupata medani katika michezo ya jumuiya ya madola.
0 comments:
Chapisha Maoni