WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI WAASWA KUPIGA VITA UKATILI WA KIJINSIA

 Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa CHAMPION Dr.Monica Magoke Mhoja akimkaribisha katikaWarsha Naibu Waziri wa Kaiba na Sheria Angela Kairuki kulia kuzindua warsha hii ya Ukatili Zidi ya Jinsia iliyofanyika katika Hotel ya Twins Park Bagamoyo jana.
 Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Angela Kairuku akifafanua maelezo kwa Wahandishi Wabari kuhusu vitendo vya Ukatili wa Kijinsia jana huko Bagamoyo.
 Mhariri toka CHANEL TEN Said Mihiko akitoa Maoni yake zidi ya Ukatili wa Kijinsia kwa Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Angela Kairuki huko Bagamoyo katika Warsha iliyofanyika katika Hoteli ya Twins Park.
Hawa ni baadhi ya Wahandishi wa Habari toka Vyombo mbalimbali wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Waziri wa Sheria na Katiba Mh.Angela kairuki 
 Mh.Waziri wa Sheria na Katiba Angela Kairuki akifanya mahojiano na Wahandishi wa Habari Bagamoyo jana.Warsha hii Iliratibiwa na Mradi wa CHAMPION.
Mh.Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na Wahandishi Wahabari toka Vyombo mbalimbali Wilayani Bagamoyo jana na kulia kwake ni Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa CHAMPION Dr.Monica Magoke Mhoja.
Naibu Mkurugenzi wa Mradi wa CHAMPION akiwa katika picha na Mkurugenzi wa Blog hii na ni mwandishi wa habari toka STAR TV Nd.Gloria Matola katika warsha ya kupinga Ukatili wa Kijinsia Bagamoyo.

Naibu Waziri wa Sheria na katiba jana alikuwa mgeni Rasmi kwenye ufunguzi wa Warsha  ya siku moja kuhusu Waandishi wa Habari na Sheria na Sera zinazohusiana na Ukatili wa Kijinsia iliyofanyika Twins Park Hotel Bagamoyo tar.10.02.2014.

Mradi huu wa CHAMPION unasaidiwa (kufadhiliwa) kwa hisani ya watu wa Marekani (USAID) kupitia PEPFAR ambao ndio waliofadhili Warsha hii.

Katika Warsha hii Mh.Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki aliwaasa Waandishi wa Habari kupinga vikali Ukatili wa Kijinsia kwa kutoa nakara katika vyombo vyao husika.Vilevile Mh.Waziri aliwaambia Waandishi kuwa wao ni msaada mkubwa kwa Serikali katika kuziwezesha jamii za Kitanzania kuacha na kujifunza athari za Ukatili wa Kijinsia ambao umekuwa kwa kiwango kikubwa nchini humu.


Aidha Mh.Waziri alieleza mikakati na sera zilizowekwa na Serikali katika kipindi hiki katika kutokomeza hali hii nchini mwetu kwa kushirikiana na Waandishi wa habari.

"Aidha ni fursa nyingine ya waandishi wa habari nchini kuweza kuonyesha umahiri katika kusaidia jamii kuelewa uwepo wa sera na sheria mbalimbali zinazowalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na hivyo kuifanya tasnia ya habari muhimili muhimu katika kupinga ukatili wa kijinsia.
 

Nimeelezwa kwamba warsha hiiitafuatiwa na warsha nyingine mbili zitakazofanyika katika mikoa ya Lindi na Mtwara.Nina imani kwamba waandaaji wamelenga kuwafikia waandishi na wahariri wa habari katika kila nyanja ya nchi yetu kwa kuzingatia nafasi yao muhimu katika kuelimisha umma

Kwa niaba ya Serikali,napenda kuchukua fursa hii kwa mara nyingine kuwapongeza Engenderhealth/Champion kwa dhti kwa kuja na wazo hili ili kuleta hamasa kwa wahariri na jamii yetu kupambana na ukatili wa kijinsia kupitia ujuzi wa sheria na ser zinazohusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia na mapungufu ya sheria na sera hizo.

Ni matumaini yangu kwamba Wahariri na waandishi wa habari mliopo hapa mtatumi warsha hii kuendelea kutoa elimu kuhusu kupinga ukatili wa kijinsia katika jamii yetu."

Hayo ndio maneno aliyowaachia waandishi na wahariri wa habari huko bagamoyo jana katika warsha ya kupinga ukatili wa kijinsia.       


                      Imechapishwa na Evance wilfred Naibu Mkurugenzi wa Blog hii.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List