Mkurugenzi
wa bendi ya muziki wa dansi Extra Bongo 'Next Level' 'Kamarade' 'wazee wa
Kimbembe' Ally Choki alijikuta akimwaga machozi baada ya watu wanaodhaniwa kuwa
vibaka kujipenyeza wakati wa uzinduzi wa albamu ya 'Mtenda Akitendewa'
iliyozinduliwa Februari 22 mwaka huu na kumuibia saa ya silva yenye thamani ya
dola 300 sawa na sh.500,000.
Extra
Bongo ilizindua albamu hiyo ndani ya Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini
Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mamia ya mashabiki na wadau wa muziki wa
dansi ambapo Choki aliingia ukumbini akiwa ndani ya gari la kubeba
wagonjwa 'Ambulance' na kulakiwa juu kwa juu.
Choki,
alieleza, tukio la kuibiwa lilimkuta wakati akishuka kwenye ambulance
ambapo ndani ya kundi la mashabiki waliompokea kulikuwepo na vibaka
waliofanikwa kumvua saa hiyo pasipo yeye kujitambua.
"Kwa
kweli saa yangu inaniuma sana nililetewa zawadi na rafiki yangu kutoka
Qatar lakini ndo hivyo vibaka wameniingiza mjini alisema Choki kwa
masikitiko na kuongeza.
"Wakati
nimepanda jukwaani ndiyo nikashtukia nimelambwa saa, bahati nzuri simu
na vitu vyangu vingine vya thamani nilikuwa nimeviacha kwa mlinzi wangu
vinginevyo hali maumivu yangekuwa makali zaidi ya hivi.
Tukio la Choki kuibiwa linakumbusha tukio jingine lililowahi kutokea miaka kadhaa nyuma kwa
aliyekuwa rapa wa bendi ya Tanzania One Theatre (TOT) Papii Kocha
'Mtoto wa Mfalme' kuporwa cheni na vibaka akiwa jukwaani wakati wa
uzinduzi wa moja ya albamu za bendi hiyo katika viwanja vya Leaders
jijini Dar es Salaam.
Aidha
Choki alisema atatoa zawadi ya sh.300,000 kwa mtu yoyote atakayeweza
kufanikisha kupatikana kwa saa hiyo huku akitaka aliyeiba kumrejeshea kiroho
safi na atampatia kiasi hicho cha fedha pasipo kufikishwa kwenye vyombo vya
dola.
"Nimeamua
kutoa zawadi kwa atakayewezesha niipate saa yangu au kwa aliyechukua
kuirudisha kwangu, hii ni sababu nilikuwa naipenda sana alieleza.
0 comments:
Chapisha Maoni