ASKARI wa magereza wa jela la Taveta Boniface Muriithi amemuua kwa kumpiga risasi mwenzake kwa jina Livingstone Sowene.
Tukio
hilo limetokea leo saa mbili asubuhi ya Jumanne lilitokea nje ya gereza
hilo wakati Muriithi alipoamua kummiminia mwenzake risasi tano kwenye
kifua bila kumuuliza chochote.
Wawili hao hata hivyo wamekuwa na uhasama ambao unadaiwa kuzidi baada yao kupangwa wafanye kazi katika shifti moja.
Mkuu
wa gereza hilo Bw Soud Ramadhan amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa
wamemnasa mwenzao huyo na kumkabidhi kwa polisi ili afunguliwe
mashtaka.
“Muriithi
alimkuta Sowene akisubiri kupeleka wafungwa kazini alipompiga risasi
tano kifuani, alikufa akiwa ameketi papo hapo. Ni jambo la kushangaza
kwa hata hawakuongea ndiposa tujue kama palikuwepo uhasama wowote,”
akasema askari huyo.
Duru
hata hivyo zinasema mshukiwa alijawa na ghadhabu baada ya kupashwa
habari kwamba askari huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mumewe.
Jamii na rafiki wa marehemu wamelalamika kumpoteza mmoja wao kwa njia katili ya kuangamizwa na mfanyakazi mwenzake.
Babake marehemu Bw Joseph Sowene amesema kuwa mwanaye aliamkia kumpeleka bintiye shuleni na mkewe shuleni Makloriti anakofunza.
“Tumetatizika
pakubwa kwa kuwa aliyeuawa ni mzazi mchanga aliyejali sana jamii yake.
Hatujui kilichosababisha hili na tunataka polisi watuambie
kilichotokea,” akalalama mzazi.
Mkuu
wa polisi wa Taita Taveta Richard Bitonga alithibitisha kisa hicho na
kusema uchunguzi unaendelea kubaini kiini hasa cha mauaji hayo.
Mshukiwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Taveta akisubiri kufikishwa mahakamani karibuni.
0 comments:
Chapisha Maoni