Issa Kipemba 'Kipemba' aliyepigana kuirejesha tena Kaole Sanaa |
Mmoja wa waasisi wa Kaole Sanaa, Bi Chuma Suleiman 'Bi Hindu' aliyecheza igizo la 'Kipusa' |
Unamkumbuka Mzee wa Mabreka? Swebe Santana naye ndani dah! |
Kundi hilo lililoasisiwa na kuundwa na wasanii wakongwe wa maigizo waliotamba kupitia Radio Tanzania (RTD) na lililokuja kutamba na michezo yao ya kwenye runinga kupitia kituo cha ITV kabla ya kuhamisa TVT (sasa TBC1) lilikuwa kama 'limekufa' hasa baada ya mastaa wake kuhamia kwenye filamu.
Hata hivyo mmoja wa mastaa wake, Issa Kipemba na wenzake kadhaa walikaa chini na kutafakari ili kulirejesha tena kwa nguvu kundi hilo.
Vikao kadhaa vilivyowahusisha baadhi ya waasisi wake kama Chuma Suleiman 'Bi Hindu' na wengine hatimaye kundi hilo limeanza kurekodi igizo lao jipya kwa ajili ya kuwarejesha burudani mashabiki wake ambayo waliikosa kwa kipindi kirefu.
Igizo hilo ambalo hata hivyo bado halijafahamika litaonyeshwa katika kituo gani cha runinga kwa sasa nchini, utafahamika kwa jina la 'Kipusa' ambapo sehemu kubwa ya tamthilia hiyo imesharekodiwa sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na MICHARAZO mmoja wa nyota wa kundi hilo Adam Malele 'Swebe Santana' alisema tamthilia hiyo imewashirikisha asilimia kubwa ya nyota za zamani wa kundi hilo.
Swebe aliwataja baadhi ya nyota hao akiwamo yeye ni pamoja na Rashid Mwinshehe 'Kingwendu', Issa Kipemba 'Kipemba', Abdallah Mkumbira 'Muhogo Mchungu' na Ndimbango Misayo 'Thea'.
"Pia igizo hilo limewashirikisha Khadija Yahya 'Davina', Bi. Star, Happiness Stancelaus ‘Nyamayao’, Mzee Chap Chapuo,Davina, Bi Star, Bi Hindu, Mama Nyamayao na wengine," alisema Swebe.
MICHARAZO ilikuwa wa kwanza kudokeza kuwepo kwa mipango ya kurejeshwa upya kwa kundi hilo baada ya kuwafumania Lango la Jiji wakifanya vikao na sasa imethibitika suala hilo ni kweli tupu.
Taarifa zaidi na wasifu wa washriki walioucheza mchezo huo MICHARAZO itaendelea kuwajuza kila mara.
0 comments:
Chapisha Maoni