kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink yawazawadia wazee wa Yombo Kilakala, Dar es salaam



 Mfanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Zabida Kibiki akimvisha shuka baada ya kumkabidhi msaada huo John Shitundu ambaye ni miongoni mwa wazee waliopo chini ya kituo chaTushikamane Pamoja Foundation wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee hao wanaoishi katika kituo hicho kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. Jumla ya vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5. Kushoto anayeshuhudia ni Mwenyekiti wa kituo hicho Rose Mwapachu.
 Meneja Mikataba wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink, Taddious Theodore akimkabidhi  msaada wa Shuka Julieth Mchanga  kwa niaba ya wazee wenzake 45,  wakati  wafanyakazi wa kampuni hiyo walitembelea kituoni hapo kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam, vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia  chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa katika picha ya pamoja na wazee wasiojiweza wa kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation ilichopo Yombo Kilakala wakati walipokwenda kuwapa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo mashuka, blanketi,vyote vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 2.5
 .Wafanyakazi wa  Kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  wakiwa na mizigo mbalimbali ya vyakula wakati  walipokwenda kutoa misaada mbalimbali kwa wazee wasiojiweza katika eneo la Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,  wanaolelewa na Kituo cha Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam. vitu mbalimbali vilitolewa  ikiwemo mashuka ,blanketi , mchere na mafuta ya chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Baadhi ya wazee wanaoishi na kutunzwa katika Kituo cha  Tushikamane Pamoja Foundation kilichopo Yombo Kilakala jijini Dar es Salaam,wakicheza pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Uwakala wa ajira ya Erolink  walipowatembelea wazee hao mahususi kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali kama vile mashuka ,blanketi , mchele na mafuta ya kupikia chakula vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 2.5.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List