Stori: Joseph Shaluwa
IMEBUMBURUKA! Kumbe
staa wa sinema za Kibongo, Wastara Juma, aliye mama wa watoto watatu,
mmoja kati yao, alizaa na mkongwe katika Bongo Hip Hop, Msafiri Kondo
‘Solo Thang’.
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika kilipasha kuwa Wastara amekaa na siri hiyo moyoni kwa muda mrefu sana.
“Mtoto mmoja alizaa na Solo, wakati ule Solo akiwa anatamba na nyimbo
zake kama Homa ya Dunia, Mambo ya Pwani na Mtazamo ambao alishirikiana
na Afande Sele na Profesa Jay. Tena leo (juzi Jumatano) ameandika kwenye
Instagram na ameweka na picha ya Solo,” alipasha shosti huyo.
Haraka paparazi wetu, akazama kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram na
kufanikiwa kuona picha hiyo iliyosindikizwa na maneno: “Baba wa baby wa
miye, Msafiri Kondo a.k.a Solo Thang, moyo wako haukupishana sana na wa
Sajuki (Juma Kilowoko).
“Sijawahi kuyasema haya lakini utazipata salamu huko ulipo. Maisha
yametutenganisha ila sijawahi kugombana na wewe wala familia yako.
Nashukuru kwa upendo wenu juu yangu hasa mama yako. Nawapenda sana na
hata mtoto wenu anawapenda. Dunia ni njia tu, hatujui nani atatangulia.
Nakutakia mafanikio. Inshallah.”
Risasi Jumamosi lilimpandia hewani Wastara ili kupata ufafanuzi juu ya
ishu hiyo ambapo alikuja juu: “Hivi kwa nini mnanifuatafuata sana
jamani? Sasa umesema umeona Instagram, kwa hiyo nikusaidie nini?”
RISASI JUMAMOSI:
Nataka kujua machache kuhusu Solo na huyo mwanaye. Mlianza lini uhusiano
na kwa nini ulikaa kimya kwa muda mrefu. Ni muhimu ufafanue hili
Wastara, maana umeweka kwenye mtandao wa kijamii na wengi wameona.
WASTARA:
WASTARA:
Naomba mniache, nina mambo mengi yananisumbua kichwani mwangu. Kama
wameona, acha waone. (Tiiii...tiii...tiiii.... Wastara alikata
simu).Chanzo:www.globalpublishers.info
0 comments:
Chapisha Maoni