Ziara
ya Mwenyekiti wa Vijana Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro Komredi
Japhar Mghamba akiongozana na Katibu Msaidizi wa Mkoa Maalum wa Vyuo
Vikuu Komredi Daniel Zenda inaendelea kwa mafanikio makubwa katika
wilaya hiyo ambapo mpaka sasa imefanikiwa kuingiza Vijana 1800 katika
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) pamoja na
Chama.
Ziara
hiyo iliyobeba jina la Operation Kokoro iliyoanza wiki iliyopita ilipata
misikosuko hasa baada ya moja ya msafara wake kushambuliwa kwa risasi
na watu wasiojulikana. Operation hiyo inayolenga kuhamasisha Vijana wa
Upinzani na wasio na vyama kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM),
kuhamasisha Vijana wa CCM kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi
ujao wa Serikali za mitaa hapo baadae October mwaka huu pamoja na
kukagua, kuhamasisha na kuelezea katika matawi na kata juu ya
utekelezaji wa Ilani ya chama kwa kauli mbiu "CCM Mwanga Ukimya sasa
Basi"
Operation
kokoro tayari imeshapita katika kata ya Kisangara, na kuendelea katika
milima ya upareni maeneo ya Ugweno, Msangeni, Kifula, Mamba na Kikweni.
Viongozi hao wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wametembelea vikundi
mbalimbali vya bodaboda, makundi ya wajasiriamali wadogo na wakubwa
pamoja na kukagua miradi iliyoainishwa kwenye Ilani ya Chama ambayo
inayoendelea kutekelezwa wilayani humo na Serikali ya Chama Cha
Mapinduzi.
Viongozi
hao wakiwa wanahutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Msangeni
wamesema kuwa wananchi waendelee kuiamini CCM kwani ndio Chama Bora Cha
siasa ambacho kinasikiliza kero za wananchi wake na kuzitafutia ufumbuzi
na kutaja kero mbalimbali ambazo tayari zimepatiwa ufumbuzi wa kudumu
wilayani humo.
Ziara hiyo inaendelea katika kata na maeneo mengine ya wilaya ya Mwanga.
0 comments:
Chapisha Maoni