PATI MAALUM LA KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE MANGO GARDEN!



-Katika kusherehekea siku ya Wanawake Jumamosi hii tarehe 08-03-2014 Bendi yako PENDWA ya Twanga Pepeta ikishirikiana na Mdau wake mkubwa Christer Bella Mwingira na Rukia Saloon, kwa pamoja wameandaa bonge la Pati kwa ajili ya kusherehekea sikukuu hii.

-Pati linataraji kufanyika ndani ya Twanga City Mango Garden ambapo muonekano wake utakuwa tofauti na siku za kawaida kwa kuwa ukumbi utapambwa vilivyo.

-Mavazi rasmi yatakuwa ni ya ya rangi NYEKUNDU, NYEUPE na NYEUSI.

-Zawadi kedekede zitatolewa na Rukia Saloon na Christer Bella Mwingira kama vitenge na Khanga ambayo ni mavazi rasmi ya mwanamke.

-Kutakuwa na ofa maalum kwa ajili ya akina mama toka kwa Mkurugenzi wetu Asha Baraka kwa kila atakayefika katika onyesho atalipia Tshs 5,000. kuanzia saa mbili mpaka saa nne usiku.

-Kiingilio kitakuwa ni Tshs 10,000. kwa VIP pamoja na kinywaji na kawaida ni Tshs 7,000/=
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List