ASIA IDAROUS AWIKA NA MAVAZI YA UBUNIFU NCHINI NIGERIA



 1-Asia Idarous akiwa na vazi la Kitanzania 

Asia Idarous akiwa na vazi maalum alilolibuni ambalo lilitia fola kwenye  onyesho hilo @ Sheraton Hotel Abuja Nigeria.

2- keki ya miaka 50 ya muungano wa Tanzania , Abuja Nigeria
Keki ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, iliyoandaliwa na watanzania, Abuja Nigeria. 
3-Fatma Mwinyi
Fatma Mwinyi akiwa kwenye pozi katika onyesho hilo la miaka 50 ya muungano Abuja Nigeria6-Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania
Asia Idarous & Teddy Mapunda @Sheraton hotel Abuja Nigeria Celebrating MuunganoTanzania

Na Andrew Chale

MBUNIFU mkongwe wa mitindo nchini, Asia Idarous Khamsin mwishoni mwa wiki aliweza kuitangaza vyema Tanzania katika onyesho  kubwa la mavazi ya ubunifu lililokuwa maalum kwa  ajili ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, lililofanyika Abuja, Nigeria.

Onyesho hilo la aina yake, lililofanyika kwenye hoteli ya Kimataifa ya Nyota  tano ya Sheraton Abuja, usiku wa  April 25,  huku likiudhuriwa na watu wengi wakiwemo watanzania na raia wengine wa kigeni walioongozwa na balozi anayewaiwakilisha  Tanzania, nchini humo Balozi Daniel Ole
Njoolay.

Akizungumza na mtandao huu, kwa njia ya simu kutoka Abuja, Nigeria,  Asia Idarous ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fabak Fashions, aliwashukuru watanzania kwa kuandaa onyesho hilo maalum,  kwani limeweza kuitangaza Tanzania kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo ya ubunifu, biashara na utalii.

“Hii ni heshima kwangu na kwa Tanzania, kwani wenzetu Wanaigeria wamevutika na bidhaa zetu nyingi zikiwemo zile tulizotumia kwenye mavazi ya ubunifu. Hivyo nasema hii ilikuwa ni nafasi ya kipekee kuwavuta kuja nchini kwa fursa za kiuchumi na uwekezaji” alisema Asia Idarous.
Alisema baadhi ya bidhaa ikiwemo khanga, vikoi, batiki na mashuka ya wamasai kutoka  Tanzania, yalitia fola na kuvutia wengi wakiwemo raia wa Nigeria na wageni wengine waliofika kwenye sherehe hizo.

Sherehe hizo mbali na kuhudhuriwa na balozi wa Tanzania, pia mabalozi mbalimbali wa mataifa wengine nao walijumuika kwa pamoja kwenye onyesho hilo.  Wengine ni pamoja na Mkurugenzi wa Montage Ltd, Teddy Mapunda, Fatma Mwinyi, Salma Maulid  na wengine wengi.
 “Utanzania wetu ni Muungano wetu, tuulinde, tuumalishe na kuudumisha  ndani na nje ya mipaka yetu, hakika onyesho hili pia litaendelea kuwa la kuongeza tija ya umoja wetu ikiwemo watanzania waishio nje ya mipaka yao ‘Diaspora’” alisema Asia Idarous.

 Nigeria ni miongoni mwa nchi pekee zenye kudumisha utamaduni wake ukiwemo wa mavazi yenye kuwatambulisha watu wa jamii hiyo, tasnia ya ubunifu na mitindo imekuwa ikipewa kipaumbele hali inayopelekea tija  na hata Taifa hilo kuwa juu kiuchumi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List