Bondia Iraq Hudu 'Kimbunga' afariki, kazikwa leo



MISIBA imeendelea kuiandama fani ya michezo na burudani baada ya alfajiri ya jana bondia nyota wa zamani wa ngumi za kulipwa, Iraq Hudu 'Kimbunga' kufariki akiwa amelazwa kwenye hiospitali ya  Hindu Mandal, Dar es Salam.
Kwa mujibu wa mpwa wa bondia huyo aliyetisha kwa ngumi nzito na kutwaa ubingwa katika ngumi za ridhaa kabla ya kuingia zile za kulimwa miaka ya 1990, Rajabu Mhamila 'Super D', Kimbunga alikuwa akisumbuliwa na tatizo la Figo na kwamba anatarajiwa kuzikwa kesho majira ya saaa saba mchana.
Super D alisema msiba wa biondia huyo upo nyumbani kwake  Buguruni Kisiwani na mazishi yatafanyika kwenye makaburi ya Kisutu.
Msiba huo wa Kimbunga umekuja wakati wadau wa michezo na burudani wakiwa bado wanaendelea kuomboleza vifo vya wasanii na wanamichezo kadhaa waliokumbwa na mauti ndani ya kipindi cha mwezi mmoja sasa.
Baadhi ya waliokumbwa na mauti kwa siku za karibuni ni wanamuziki Muhidini Mwalimu Gurumo, Amina Ngaluma 'Janapese', Recho Haule, Adam Kuambiana, George Tyson, Mzee Small, Abdallah Sumbwa, Ally Mwanakatwe na nahodha wa zamani wa KMKM ya Zanzibar.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List