Meneja
Biashara Kanda ya Ziwa Raphael Daudi (wa tatu kutoka kulia) akiwa na
Meneja wa Masoko Kanda Emanuel Raphael (wa kwanza kulia) pamoja na
Meneja wa Airtel mkoa wa Mwanza David Wankulu wakikabidhi msaada wa
chakula cha kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kwa
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Kuendeleza Quran na Suna Tanzania (JUQUSUTA)
Twaha bin Bakari Utari (wa tano kutoka kulia) akiwa katika picha na
wadau wengine wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith
kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
|
Vijana
wa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said Al-Bith kilichopo eneo la
Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza wakishusha vyakula toka katika gari
la wadau wa Airtel ambao wamedhuru katika kituo hicho kwaajili ya
kusababisha tabasamu kwa watoto hao kwa kipindi hiki cha mfungo wa Mwezi
mtukufu wa Ramadhani..
|
Upakuaji ukiendelea.
|
Ni
sukari, chumvi, majani ya chai, mchele, sabuni, mafuta, unga wa sembe,
unga wa ngano, juice za matunda na vinginevyo kama sehemu ya msaada wa
chakula toka Airtel Tanzania kwa Kituo cha watoto yatima cha Sharif Said
Al-Bith kilichopo eneo la Nyegezi Majengo Mapya jijini Mwanza.
|
0 comments:
Chapisha Maoni