Mmoja wa mtumishi walioshtakiwa na CCBRT
Mmoja wa mtumishi walioshtakiwa na CCBRT
.
Vijana hao wameongea na vyombo vya habari juu ya kesi yao kwa kutoa malalamiko ya kutaka kufukuzwa kazi kinyemela kutokana na kubinifsishwa kwa kitengo hicho cha viungo bandia kisili.Pia wameshangazwa na taratibu ya kila mmoja kufunguliwa namba yake ya kesi wakati ni kesi moja.CCRBT ambao ni washtaki wa kesi hiyo wametumia kigezo cha Elimu kuwa ni Degree tu na sio DIPLOMA au Certificate kutokana na mahitaji ya mfadhili mpya NA viwango vya W.H.O(WORLD HEALTH ORGANIZATION) na I.S.P.O (International society for Prosthetics and Orthotics) ambapo pia vijana hao wakijibu wanasema'wao wanaye mtambua ni mwajili wao CCBRT na sio Mfadhili'
Kigezo hicho ambacho kimechukuliwa kama kikubwa kimepingwa vikali kutokana na Vijana hao kuajiliwa na kufanya kazi katika kitengo hicho kwa zaidi ya miaka mitano na Wengine wamefikisha zaidi ya Miaka kumi ndani ya kitengo hicho hivyo kwao ni kigezo ambacho hakina mshiko na Uonevu dhidi ya Wananchi wa Tanzania unaofanywa na Wageni toka nchi za nje.Pia kama Kigezo ni Elimu' kwa nini wasipatiwe Elimu na mwekezaji ili kuendeleza watanzania na si kuwatelekeza wafanya kazi wa ndani na kuwapa kipaumbele wageni toka nje'.
Mwisho wametoa malalamiko kwa bodi ya CCBRT(Comprehinsive Community Based Rehabilitation in Tanzania) kwa kufumbia macho na kushindwa kufanya jambo lolote kuwatetea ili kupata haki yao.Bodi ya CCBRT ambayo ipo chini ya Dr.Willbord Slaa imenyamazia suala hilo bila kutoa ushirikiano wowote kwa Vijana hao.
Picha ya mgonjwa anayepatiwa huduma na vijana hao waliofukuzwa kazi.
Hapa baada kuwekwa viungo bandia
baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa huduma ya viuongo bandia
0 comments:
Chapisha Maoni