Wakazi waishiyo Kimbiji wilaya ya Temeke jijini Dar es salaam wameiomba Serikali isikie kilio chao,wapo katika hali ngumu ya maisha baada ya kufungwa kwa kituo cha mafuta Oil Link ambapo walikuwa wakipata huduma ya mafuta ya taa,Petroli,Dizeri nk. hivi sasa kimefugwa.Wananchi hao wamedai asilimia kubwa wanaoishi na wenyeji wa Kimbiji ni wenye kipato kidogo cha chini nyumba zao azina umeme wanaishi kwa kutumia Koroboi,kufungwa kwa kituo hicho itasababisha uwalibifu wa mazingira kwa kukatwa miti hovyo ili iwasaidie kwa kutumia Limuli kuangazia ndani, uwezo wa kufata mafuta ya taa Kivukoni kigamboni gharama ya nauli ni kubwa ukilinganisha na uwezo duni waliokuwa bao.
Wananchi hao wakizidi kulalamika wamesema wanaishi kwa kutegemea kazi za uvuvi wakati huo Boti,Mitumbwi,Karabahi zinategemea mafuta ili waweze kuwajibika katika shughuli zao za uchumi,hivyo wako katika hali ngumu ya maisha na wameiomba serikali isikie kilio chao, pamoja na kutengenezewa kwa barabara ya kutoka Kivukoni Pemba mnazi Kimbiji kwa kuwa hiko katika hali mbaya wanatumia gharama ya nauli kubwa kutokana na kuwa na magari yanayoenda huko ni machache kutokana na hali mbaya ya barabara.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kwa Chale bwana, Silvery Kalikisha amesema wapo katika hali ngumu ya maisha kwa kukosa miundombinu ya barabara bora pamoja na kufungiwa kwa kituo hicho cha mafuta wananchi wapo katika hali mbaya ya uchumi kwa kuwa wanatumia muda mrefu kwenda kutafuta kuni za kupikia na kuwasha Limuli wakati wa usiku,Limuli hutumika kama Toch ya kumulikia ndani kupata mwangaza
Naye msimamizi wa Kituo cha Mafuta Oil Link bwana Karine Mmadi amesema kituo hicho Kimefungiwa na Ewura kwa madai ya Kukosa Kalo walielekezwa na kuambiwa wakitengeneza watoe ripoti watakapo lidhika watafunguliwa na kuendelea na shughuli zao,walitimiza na kufanya hivyo lakini walipofika wakai wachimbe Kalo lingine wametekeleza wamefika kuona lakini kimya awajui tatizo liko wapi
Diwani wa kata ya Kimbiji Mhe Muhdini Bunanyasana ameungana na wananchi wake kuiomba serikali isikie kilio chao kituo cha mafuta Oil Link kifunguliwe ndio mkombozi wa Kimbiji Kiuchumi.wananchi wake wamejiajiri sekta binafsi wanaendesha Pikipiki na Uvuvi wakitegemea kupata mafuta katika kituo hicho pia swala la barabara mbovu itengenezwe kwa sababu wamiliki wa magari awataki kupeleka magari yao sababu utozwa nauli kubwa kulingana na miundombinu mibovu.
Barabara ya kimbiji jinsi ilivyoalibika.
0 comments:
Chapisha Maoni