Mashindano
ya kumsaka mrembo kanda ya Mashariki ( Redds Miss Eastern Zone 2014)
yatafanyika siku ya sikukuu ya Nanenane kwanue ukumbi wa Nashera Hotel, mkoani Morogoro.
Mashindano
hayo yatashirikisha jumla ya warembo 14
kutoka mikoa minne ambayo ni Pwani, Lindi, Mtwara na mwenyeji, Mkoa wa Morogoro
chini ya udhamini wa Redds Original, Zanzi Cream Liquer, Pepsi, Usambara Safari
Lodge, Kitwe General Traders, Starwing Lodge, Nashera Hotel, CXC Africa, Sykes
Travel, Sasa Saloon, Grand Villa Hotel, Shabibi Line na Clouds FM.
Mratibu
wa masindano hayo, Alex Nikitas aliwataja warembo watakaoshindana siku hiyo
kuwa ni Lucy Julius Diu, Prisca Mengi,
Tarchisia Noback Mtui na Angel Shio
ambao wanatoka Morogoro.Warembo
wengine ni Elizabeth Tarimo, Lilian Andrew
na Leila Abdul Ally ambao wanatoka mkoa wa Lindi ambapo
kutoka Mtwara ni Nidah Fred Katunzi, Lightness
Mziray na Nelabo Emmanuel.
Pia
warembo kutoka Pwani ni Khadija Ramadhan Sihaba, Irene Rajabu Soka, Mary Mpelo na Arafa Shaban. Nikitas alisema kuwa
warembo hao watakuwa kambini kuanzia Julai 29 kwenye hotel ya Usambara Safari
Lodge chini ya Miss Kanda ya mashariki mwaka jana, Diana Laizer.
0 comments:
Chapisha Maoni