Naibu Waziri Mh.AMOS MAKALA akikagua maendeleo ya mradi wa maji maeneo ya chuo kikuu Dar es salaam
NAIBU Waziri Wa Wizara Ya Maji,Amosi Makala, amevifungia viwanda vya uzalishaji matofali Motto Company LTD kilichopo maeneo ya Ubungo,ujenzi solving, kwa kosa la kujiunganishia Maji kiholela.
Makala alichukua hatua hiyo jana, alipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi miwili ya maji, inayosimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na maji taka, Dar es salaam, (DAWASA).
Akizungumza katika maeneo aliyotembelea kukagua ya Ubungo Maji na Kimara Msuguli, Waziri huyo alisema, baada ya kufanya uchunguzi wamegundua kuwa, viwanda hivyo,vinatumia maji ya wizi kuzalishia matofali hayo .
‘’Hatuwezi kukubali kuona wizi wa maji, ukifanyika kihololela, hivyo navifungia hivi viwanda, mpaka sheria itakapochukua mkondo wake’’,alisema naibu waziri wa maji Amosi Makala.
Makala alisema kuwa pia wamebaini viwanda hivyo vinafanya kazi katika maeneo hayo , bila vibali vya kufanyia biashara hivyo ni wahujumu huchumi na ni wezi kama wezi wengine.
‘’Tumekuwa tukifanya biashara hii tangu mwaka 2012, na DAWASCO walishawahi kuja kuangalia, hawakuona kama kuna maji yao tuinayotumia, hivyo hatukuwa na shaka juu ya hilo’’, alisema mmoja wa watuhumiwa wa wizi wa maji.
Tarimo alielezea masikitiko yake kuwa, kusimamishwa kwa kiwanda hicho, kampuni hiyo itapata hasara ya kiasi cha Sh. Milioni 90, kwa mwezi, na kupoteza hajira za wafanyakazi 20, walioko kiwandani hapo.
Alisema kuwa kampuni hiyo uzalisha matofali 2000 kila siku, ambapo utumia maji lita 3000 kutoka mto msewe, ambapo chini yake kuna mabomba ya DAWASCO yamepita.
Hata hivyo Tarimo alisema kuwa, inawezekana kuna mabomba ya DAWASCO yamepasuka, lakini wao hawana uhakika kwani licha ya kufanyiwa uchunguzi, hawakugundulika na hilo.
Mwisho.
Mbunge wa Jimbo la kawe wa kwanza kulia Mh.Halima Mdee na Naibu waziri wa Maji Mh.Amos Makala wa mwisho kushoto na mtaalamu wa maji katikati wakijadiliana mipango ya kuboresha miundombinu ya maji.
Mbunge wa Kibaha vijijini Mh.Hamed Abdul Jumma akiwa katika kuhakikisha mradi wa Bomba kubwa unaondelea kujengwa katika ziara ya Naibu Waziri wa Mh.Amos Makala
Watuhumiwa waliokamatwa kwa kesi ya kuhujumu(wizi)wa miundombinu ya maji.
Watuhumiwa waliokamatwa kwa kesi ya kuhujumu(wizi)wa miundombinu ya maji.
Naibu Waziri akitoa kauli juu ya hatua kali za sheria zitakazo chukuliwa kwa wote wanahohujumu(wizi) wa maji na waharibifu wa miundombinu ya maji.
Gari linalotumiwa kubeba maji kinyume na taratibu za kisheria
Kijiko kikiendelea na ukarabati wa miundombinu ya maji ili kuboresha na kutatua tatizo la maji Pwani na Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni