Mzee
Yusuph (Katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na Meneja Wake Said
Mwangushi (kulia) na Meneja Masoko wa Proin Promotions Limited, Evans
Stephen (Kushoto) mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa Habari
leo katika ofisi za Kampuni ya Proin Promotions Limited zilizopo Mtaa wa
Ursino Mikocheni
Mzee
Yusuph akibadilishana Mkataba na Mwanasheria wa Kampuni ya Proin
Promotions Limited Halima Mara baada ya Kumaliza kutiliana saini katika
Mikataba.
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited
Hatimaye
Mzee Yusuph atambulisha rasmi ujio wake katika Tasnia ya Filamu leo
mara baada ya kuitambulisha filamu yake mpya na ya Kwanza iitwayo
NITADUMU NAE ambapo filamu hiyo ni moja ya filamu ambazo zimetoka katika
nyimbo zake.
Akiongea
na Waandishi wa Habari Mzee Yusuph alisema "Filamu hii nimeitengeneza
muda mrefu sana na imetoka katika nyimbo zangu lakini nilishindwa
kuisambaza kutokana na kukosa Msambazaji ambaye anaweza kukubaliana na
vigezo vyangu lakini Kwa bahati nzuri Proin Promotions imeweza kuwa na
vigezo ambavyo mimi nimekubaliana navyo na nimeridhika navyo ndio maana
nimeona wanaweza kusambaza filamu yangu"
Na Pia
ameelezea sababu kubwa ya yeye kuamua kufanya kazi na Proin Promotions
ni kwamba "Kampuni ya Proin Promotions hainunui hakimiliki za wasanii
ndio maana nimeona nifanye nao kazi"
Vilevile
Filamu ya Mzee Yusuph ishaingia sokoni leo na inasambazwa na Kampuni
mahiri ya Proin Promotions Limited ambapo filamu hiyo inapatikana Nchi
nzima kuanzia leo.
Mbali
na hiyo pia Mzee Yusuph amesema kuwa sasa anabadili nyimbo zake kwenda
kwenye filamu kwasababu nyimbo zake zote zina uwezo mkubwa wakuwa filamu
ndio maana kwa kuanza ameanza na Nyimbo yake ya Nitadumu Nae.
0 comments:
Chapisha Maoni