Msingi wa jina umetokana na mtandao(Blog)iliyojulikana kwa jina hilo kwa kutoa taarifa za Handeni lakini hivi taasisi hiyo inafanya kazi nchi nzima.Sasa taasisi ipo katika mkakati wa kupata wataalamu wa kufanya utafiti,sekta ya elimu,sekta ya afya na maji.Lengo ni kufanikisha malengo yaliyokusudiwa.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh:MULHINGO RWEYEMAMU akiongea katika Utambulisho wa Handeni kwetu foundation amesema kuwa, utafiti ni kitu cha msingi sana katika kutatua matatizo ya jamii.Na amesema pia hilo lilisaidia hata kuinua elimu ya Wilaya ya Handeni na kutokomeza tatizo la mimba za utotoni.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh:MULHINGO RWEYEMAMU ameongeza kuwa atakuwa tayari kushirikiana na taasisi hiyo na kutoa ombi kwa wananchi wote kutoa ushirikiano.Naye Mwenyekiti Ndugu Adam Malinda amesema taasisi hiyo itaanza na Handeni na baadeye itajitanua zaidi Tanzania.
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh:MULHINGO RWEYEMAMU
Mwekiti wa kwetu foundation ndugu,ADAM MALINDA
KIKUNDI CHA NGOMA KIKITOA BURUDANI
Wadau wa maendeleo wakifuatilia kwa makini tukio la Utambulisho wa Handeni kwetu Foundation
0 comments:
Chapisha Maoni