KIRAKA wa klabu ya Azam na timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Erasto Nyoni usiku wa kuamkia leo, alimbwaga nahodha na beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ katika tuzo za mwaka 2013/14 katika kipengele cha mchezaji bora wa soka wa kitaifa.
Katika tuzo hizo zinazoandaliwa na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), zilifanyika kwenye
Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar na Nyoni kufanikiwa kuitwaa kwa
kuwagaragaza Cannavaro na straika wa Simba, Elias Maguli ambao
walifanikiwa kuingia hatua ya fainali.
Kwa upande wa tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, nyota wa Azam, Muavori Coast, Kipre Herman Tchetche aliwabwaga Mrundi, Amisi Tambwe wa Simba na beki wa Yanga, Mnyarwanda, Mbutu Twite.
Mbali na tuzo hizo, shujaa katika tuzo hizo alikuwa ni straika yosso wa timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’, Sheridah Boniface ambaye alitwaa tuzo tatu mfululizo ikiwa ni rekodi ya aina yake tangu tuzo hizo zianzishwe mwaka 2006.
Sheridah ambaye mwaka jana alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa michuano ya Afrika ya wanawake ya Airtel Rising Stars iliyofanyika nchini Nigeria, usiku wa jana aling’ara kwa kutwaa tuzo ya Wanamichezo chipukizi akiwangusha Omary Sulle (tenisi) pamoja na kipa wa Azam, Aishi Manula.
Kinda huyo mwenye miaka 17, aliibuka tena kidedea kwenye tuzo ya mchezaji bora wa wanawake akiwazima Sophia Mwasikili na Amina Ally huku pia akitwaa tuzo ya jumla.
Wachezaji wanaocheza nje ya nchi, Mbwana Samatta anayekipiga TP Mazembe ya DR Congo aliondoka na heshima hiyo kwa ‘kuwakalisha’, Thomas Ulimwengu ambaye wapo timu moja pamoja na mwendesha baiskeli Richard Laizer aliye Afrika Kusini.
Tuzo nyingine ni: Francis Cheka (Ngumi za kulipwa), Seleman Kidunda (ngumi za ridhaa).

(Habari/Picha: Musa Mateja/GPL)
0 comments:
Chapisha Maoni