Mratibu wa mpango mpya wa Steps Entertainment, myovela Mfwaisa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na mwongozaji wa Filamu nchini, Jackob Steven 'JB' akizungumzia ujio mpya wa Steps.
Wakionesha Makasha mapya ya muvi za kibongo zitakazoanza kusambazwa na Steps mwaka 2015
Na Mwandishi wetu
Kampuni ya usambazaji wa filamu bora Tanzania ya Steps Entertainment Ltd
inatarajia kutoa bidhaa mpya za filamu kwa mwaka ujao wa 2015 filamu
zenye ubora muonekano mzuri huku pia kuwaletea walaji bei rafiki kutoka
kampuni bor a ya usambazaji wa filamu Tanzania Steps Entertainment Ltd.
Steps
Entertaiment Ltd ni ilioanzishwa mwaka 2007 nchini Tanzania na makao
yake makuu yako jijini Dar salaam, Kampuni ya Steps Entertainment
inajishughulisha na usambazaji wa filamu za Kitanzania maarufu kwa jina
la BONGO MOVIES
Tangu
kuanzishwa kwake Kampuni ya Steps Entertainment imekuwa mdau mkubwa
katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania na mpaka sasa ndiyo
kampuni kubwa ya usambazaji wa filamu nchini Tanzania.
Kampuni
ya Steps Entertainment kupitia mikakati yake ya kuinua tasnia ya filamu
nchini Tanzaania imefanikiwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa
tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu, Waigizaji, Wasambazaji
wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja na wanaoonyesha na au kukodisha
katika vibanda.
Akiongea na wanahabari Carlos Johns Silondwa mtendaji mkuu ameielezea
Steps Entertainment imefanikiwa pia kuvuka mipaka na kufikisha sinema
za kitanzania katika mataifa mbalimbali ya nje na katika luninga za
kimataifa na televisheni za ndani kuonyesha kazi za nyumbani.
“Kwa
sasa mataifa mengi Ulaya na nchi za Scandinavia wanajifunza Lugha yetu
ya Kiswahili kupitia filamu zetu, moja kwa moja utaona njia nyingine
katika kukuza Kiswahili nje ya nchi kwa njia ya filamu tu ambazo
zinasambazwa na kampuni hii, na kutengeneza ajira kwa vijana wengi,”
Pia
kampuni imekuja na bei rafiki kwa mlaji baada ya kilio chake kuumiza
kwa muda mrefu, kampuni kwa kutumia wataalamu pamoja na wadau wa filamu
kutoka sehemu mbalimbali wamefanya utafiti ili kupata Mwarobaini wa
Maharamia wa kazi za nyumbani kampuni imeshusha bei.
Hiyo
inatokana na hali halisi filamu inatakiwa imfikie mtumia kwa 6,000/
lakini utafiti umebaini kuwa mtanzania anatumia zaidi kiasi cha 34,000/
na zaidi bila kuimiliki Dvd hiyo, baada ya Vibanda au Library
kuanzimisha, badala ya kumuuzia.
Filamu
ambayo itauzwa ikiwa katika ubora na muonekano mzuri, inakuja baada ya
filamu kutoka nje, kuuzwa kwa bei ya chini kabisa na kuleta ushindani
pamoja na kuwa sinema hizo hazilipiwi kodi tofauti sana, nakuzifanya
zinunulike sana kuliko filamu za ndani kutokana na bei yake kuwa ndogo.
Kampuni
ya Steps Entertainment ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu
zinatoka mbali na bado zinawafikia walaji kwa bei ya chini ni baada ya
utafiti huo ndipo Kampuni ya Steps Entertainment iliamua kujibana na
kufanikiwa kuingiza na kufunga mtambo mkubwa wakisasa kuzalisha cd/dvd,
kuzirekodi na kuziprinti hapa hapa nchini.
Tofauti
na siku za nyuma ambapo ilikuwa inaagiza cd/dvd kutoka nje ya nchi na
kuja kuzirekodi tu, sambamba na mtambo huo pia kampuni hii imeamua
kubuni kifungashio kipya yaani kasha za cd/dvd, ambayo ni za bei nafuu,
zinamuonekano mzuri zaidi, ni rahisi kuhifadhi, nirahisi kusafiriha na
nirafiki wa mazingira.
Mtambo
mkubwa na wakisasa pamoja na kifungashio kipya vimepunguza sana gharama
za kuzalishia nakala za dvd na cd na hivyo Steps imeona ni vyema
kuonyesha moyo wa uzalendo kwa wateja wake kwa kuwapunguzia bei ya
kununua filamu kwa kuwauzia kwa nusu ya bei ya awali.
Kampuni
ya Steps Entertainment inaamini kuwa kitendo cha kupunguza bei za
filamu zake, kitawanyima Maharamia ulafi na wizi wa wazi kabisa, kama
kampuni inakaribisha wadau wote wanaosambaza filamu kwa kuja kwetu
kuzalishiwa filamu zao kwa bei rahisi sana ili huyu Gaidi mkubwa
anayenyonya kazi zetu aache.
- Kinaonyesha moyo wa uzalendo lakini pia kitapandisha mauzo ya filamu za kitanzania ambapo kwa ujumla wake itaongeza kipato kwa wasanii na kuchangia pato la Taifa.
- Kitapunguza uharamia wa filamu kwa kuwa bei itakuwa chini hivyo kila mtu atakuwa na uwezo wa kununua nakala halisi.
- Kitaziwezesha library zinazokodisha filamu kuacha kukodisha na badala yake kuanza kuuza moja kwa moja
Hivyo
basi Kampuni ya Steps Entertainment inamaliza mwaka 2014 na kuingia
mwaka 2015 kwa kubororesha bidhaa zake, zikiwa katika ubora na muonekano
wa kuvutia kwenye kasha la bahasha ngumu, bidhaa hizi zitamfikia mlaji
kwa bei ya 1,500/= tu bei hii kwa filmu zitakazo kuwa katika
kifungashio kipya pekee filamu zitakazo kuwa katika kifungashio cha
zamani yaani kasha la plastiki zitaendelea kuuzwa kwa bei ile ile na
wateja watakuwa huru kuchagua aina ya kifungashio pale wanaponunua
nakala za filamu za Steps
Hivyo basi Steps Entertaiment imeanzisha kampeni maalum ya “Faidika na Steps kwa bidhaa bora, Wasanii nyota, na Filamu Bora”.
Kampuni
ya Steps Entertainment inawaomba wadau wote kuendelea kuzienzi filamu
za kitanzania ili kukuza kipato cha wasanii na taifa kwa ujumla ,
kutangaza lugha ya Kiswahili na utamaduni wa kitazania.
Bei
zetu zitakuwa wazi kwa maan za steps tofauti ya bei iliyoandikwa kwenye
kasha ya kuonekana zikiwazimeandikwa katika kasha na mwananchi
asikulaghai mtu wa Library eti usinunue hadi hakukodishe sema No.
Mwisho,
Tunaiomba Serikali Chini ya Rais wetu Mpendwa Mheshimiwa Dr. Jakaya
Mrisho Kikwete wawasaidie wadau wa filamu kupambana na uharamia wa
filamu ambao kwa sasa umevuka mipaka wezi wanafanikiwa wasanii wanabaki
Maskini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA Mungu bariki Afrika
Carlos Johns Silondwa
Mtendaji Mkuu.
0 comments:
Chapisha Maoni