Mkurugenzi wa Huduma za Kutuma na Kupokea
Fedha wa Tigo Andrew Hodgson (wa pili kulia) akipongezana na Mkurugenzi
wa Huduma za Kutuma na Kupokea Fedha wa ZANTEL Hashim Mukudi mara baada
ya kutangaza ushirikiano kati ya huduma zao za TigoPesa na EzyPesa
mapema leo Zanzibar. Kutoka kushoto ni Meneja wa Biashara wa ZANTEL
Zanzibar Mohamed Mussa, Meneja Miradi wa ZANTEL Shinuna Kassim na Meneja
Chapa wa Tigo William Mpinga (kulia).
…………………………………………………………………………………………..
Kampuni za simu za mkononi za Tigo na ZANTEL zamezindua rasmi
huduma za kutumiana pesa miongoni mwa wateja wake Tanzania. Mbali na
huduma hiyo ya kutumiana pesa miongoni mwa wateja wa mitandao hiyo,
wateja wa EzyPesa na TigoPesa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa kwa
marafiki na ndugu walio katika mitandao hiyo popote pale nchini.
Kutekelezwa kwa mpango huo kunazifanya Tigo na ZANTEL kuwa
viongozi wa huduma kama hiyo Duniani. Haya ni matokeo ya makubaliano
yaliyotangazwa mwanzoni mwa mwaka huu na EzyPesa, TigoPesa na Airtel
Money.
Jinsi Huduma hiyo inavyofanya kazi:
Wateja wa Zantel: Wateja wa Tigo:
1. Piga *150*02# 1. Piga *150*01#
2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa) 2. Chagua: Chaguo la 1 (Tuma Pesa)
3. Chagua: Chaguo la 2 (Tuma TigoPesa) 3. Chagua: Chaguo la 5 (Tuma EzyPesa)
3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa 3.1. Ingiza Namba ya TigoPesa
3.2. Ingiza Kiwango 3.2. Ingiza Kiwango
3.3. Ingiza Neno la Siri 3.3. Ingiza Neno la Siri
3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno 3.4. Subiri Uthibitisho wa Ujumbe Mfupi wa Maneno

Hakuna gharama za ziada mteja anapotuma pesa kwa mtandao
mwingine isipokuwa gharama zinakuwa sawa na zile anapotuma kwenye
mtandao wake. Wateja wanaopokea pesa kutoka mtandao mwingine wanaweza
kutoa pesa kwa wakala wa mtandao wao na hapatakuwa tena na ulazima wa
mteja kutafuta wakala wa mtandao wa mtu aliyemtumia pesa.
Akizungumza kutoka Zanzibar, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha
wa Tigo, Andrew Hodgson alisema: “Tunafuraha kupanua wigo kwa wateja
wetu kwa ubia na Zantel. Hatua hii ni muhimu hasa kwa Zanzibar ambapo
fursa ya kukua kwa huduma za fedha kwa mitandao ya simu bado ni kubwa.”
Anasema kama ilivyo kwa huduma nyingine za simu kama milio ya sauti na ujumbe mfupi wa maneno, kuna fursa kubwa ya kuimarisha huduma kwa wateja kwa kushirikiana badala ya kushindana baina ya wadau katika sekta ya mawasiliano kwa kupanua huduma za kutuma na kupokea fedha kwa kutumia mitandao Tanzania.
Anafafanua zaidi kuwa kwa kufanya kazi na wadau wengine, kunawawezesha kupanua wigo wa wateja na hivyo kwa pamoja kutoa huduma ambazo ni bora zaidi, salama, na za haraka kwa wateja wa pande zote.
“Ubia ambao tumeingia leo sio tu utaleta karibu kampuni zetu, bali muhimu zaidi ni ukaribu wa wateja wetu kwa kuwapatia huduma za fedha za kielektroniki bora zaidi ambazo hawakuweza kuzipata hapo awali,” alisema Hodgson.
Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel, Mohamed Mussa, anasema Zantel inaendelea kutimiza ahadi ya kuwarahisishia huduma za fedha wateja wake kwa kufanya kazi pamoja na Tigopesa.

“Kwa kufanya hivi tunapanua wigo kwa wateja wetu, huduma hii
inawawezesha zaidi wateja kutuma na kupokea fedha kwa urahisi zaidi,”
anasema.
Anafafanua zaidi kuwa kwa huduma hii itasaidia kuimarisha huduma za fedha kati ya visiwa vya Zanzibar na Tanzania Bara.
“Zantel iko katika mstari wa mbele kuhakikisha kuwa ushiriki wa
wananchi wa Zanzibar katika sekta muhimu ya fedha unaimarika na kukua.
Tumehakikisha kuwa mtandao wa mawakala wetu na watoa huduma wengine wako
tayari kuwahudumia wateja wetu,” anasema Bw. Mussa.
0 comments:
Chapisha Maoni