Baada
ya ghasia na maandamano ya miezi kadhaa, hatimaye raia nchini Burundi
sasa wamefika katika vituo vya kupiga kura ili kumchagua rais wao.
Watu wawili wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu Bujumbura. Mwaandishi wa BBC aliyeko nchini humo
anasema kuwa, milio ya risasi na gruneti imesikika usiku kucha katika
mji mkuu wa Burundi- Bujumbura.
Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo anawania muhula wa 3 kama rais licha ya madai kuwa anakwenda kinyume na katiba ya nchi. Viongozi wanne wa upande wa upinzani wameapa kususia uchaguzi huo.
Rais
Pierre Nkurunziza, akiwaamevalia jezi ya michezo alipiga foleni katika
kituo kilichokaribu na mji wa Ngozi alikozaliwa na kupiga kura. Waangalizi wachache mno wanashiriki uchaguzi
huu baada ya serikali ya Burundi kuwanyima vibali waangalizi wa Umoja
wa Afrika katika muda wa lala salama.
Hata hivyo, waangalizi kutoka umoja wa Afrika Mashariki wapo huko kwa mwaliko wa rais Nkurunziza. Karatasi za kura zinaonesha kuwa kulikuwa
na wagombea nane wa kiti cha urais lakini wanne kati yao
wameshathibitisha kuwa hawatashiriki uchaguzi huo wakipinga hatua ya
rais Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Wagombea hao ni Agathon Rwasa, Jean Minani, Domitien Ndayizeye na Sylvestre Ntibantunganya. Jina la rais Nkurunziza na ishara ya chama chake imechapishwa miongoni mwa wagombea wa urais.
Saa
chache tu kabla ya kufunguliwa shughuli ya upigaji kura, milipuko ya
gruneti iliripotiwa jijini Bujumbura na kufuatiwa na milio ya risasi. Katika maeneo mengine risasi zilisikika kwa wingi zaidi mjini humo.
Japo haikuwa wazi ni nani hasa anayefyatua risasi hizo. Kwa mujibu wa mshauri wa kisaisa wa rais, haya ni mashambulio yanayofanywa na 'magaidi' wanaonuia kuvuruga shughuli ya uchaguzi.
Hofu
ya kuwa uchaguzi huu huenda ukalitumbukiza taifa hilo katika mzozo
mbaya zaidi wa kisiasa imeifanya jamii ya kimataifa kuitisha kuahirishwa
kwa uchaguzi na kupendekeza mashauriano ya amani. Wito kama huu uliambulia patupu, mwishoni
mwa wiki mashauriano ya amani yalivunjika na uchaguzi ndio huu
unafanyika huku wito wa kuahirishwa kwake ukipuuziliwa mbali.
Takriban
watu 70 wamefariki katika maandamano ya awali kupinga uchaguzi huu huku
wengine zaidi ya elfu 160 wakiikimbia nchi kwa hofu ya kuzuka mapigano.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Chapisha Maoni