Shule ya Msingi Jeshi la wokovu ya jijini Dar es salaam,inayotoa Elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum,ina upungufu wa walimu wa Sayansi na hisabati kwa muda mrefu hivyo imeiomba serikali kuwasaidia watoto wenye uhitaji ili wapate elimu.
Hayo yamesemwa wakati wa kupokea msaada wa Baiskeli na Fimbo kwa watoto wenye ulemavu wa macho na miguu Kutoka kwa taasisi ya Mohamed Punjan Foundation ya nchini CANADA.
Meja Wilson Chacha ni Mkurugenzi wa shule ya Jeshi la wakovu ameshukuru msaada huo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaosoma katika shule hiyo huku wazazi wao wakiwa hawana uwezo.
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mohamedi Punjan amesema wameguswa na matatizo mbalimbali ya watoto wenye ulemavu na kuamua kufika Tanzania kwa ajili ya kutoa msaada katika taasisi hiyo.
Taasisi ya Mohammed Punjan Foundation ya Kutoka nchi ya CANADA wamefika Tanzania kwa lengo la kusaidia watoto wenye ulemavu wa miguu na kuwapa Baiskeri za kutembelea pamoja na fimbo.Pia wametoa msaada kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa kuwapa msaada wa zaidi ya milioni 60.
MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU BAKARI MACHUMU AKUTANA NA WANABLOGU
NA WAZALISHAJI MAUDHUI MTANDAONI IKULU DAR
-
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akiwa na
viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa
Mtandaoni, pa...
Saa 17 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni