Wananchi wa mtaa virobo kata ya Chanika wamekuwa wakipata Huduma ya matibabu kwa wakati wa usiku kwa kutumia mwanga wa simu kutokana na kukosekana kwa umeme katika Zahanati ya Yangwe iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam.
Kutokana na hali hiyo wadau wameombwa kusaidia kupatikana kwa umeme wa TANESCO kutokana na umeme uliopo wa jua kutokidhi ya mahitaji hospital hiyo.
Daktari wa zahanati ya Yongwe Ally Malika ameshukuru chama cha mapinduzi Wilaya ya Ilala kwa kuwapatia umeme wa sola.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala ndugu Kafuge Joel amewataka wananchi kuwa na subira sababu chama cha mapinduzi kinataka kuendelea kutekeleza Ilani kwa vitendo.Naye Mwenyekiti wa Mtaa akiongea amesema Serikali itahakikisha inaleta umeme katika Zahanati hiyo.
Licha ya kuwa Zahanati hiyo imesaidiwa umeme ila bado lina changamoto ya maji na upungufu wa wahudumu.
DKT. KIJAJI ASISITIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KATIKA UHIFADHI
-
Na Kassim Nyaki, Karatu.
Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameelekeza
taasisi za uhifadhi kuimarisha matumizi ya teknolojia za k...
Saa 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni