Wahitimu wa fani ya Ualimu waendelea kuilalamikia Serikali kwa kushindwa kutoa ajira za walimu kwa muda unaofaa na kushindwa kutoa taarifa yoyote juu ya Lini hasa ajira hizi zitatoka.
Akiongea na mwandishi wa Blog Mwenyekiti wa wahanga wa ajira 2015/2016 ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Mapindizi ndugu Stuart George ameiomba Serikali kutoa ajira mapema ili kutimiza ahadi walizoweka kwa wananchi ikiwemo suala la ajira za walimu sababu linagusa maisha ya watu wengi.Kiongozi huyo aliyegombania ubunge pia kwa tiketi ya ccm jimbo la mbagala kura za maoni amesema Chama kinahitaji kushawishi ajira hizi zitoke sababu kuna kundi la vijana zaidi ya laki moja ambao ni wapiga kura na wanaendelea kuchoshwa na hali hii.
Pia amewaomba wahitimu wote wahanga Kumuombea Dkt Magufuli ili afanikishe ahadi zote sababu ni Msikivu na tunaona anawasaidia watu wa hali ya chini kama machinga.
NGORONGORO LADIES MGUU SAWA MASHINDANO YA SHIMMUTA MOROGORO
-
Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na
program ya...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni