Wahitimu wa mafunzo ya ufugaji samaki wa CHUO cha Mbegani,Wilaya ya Bagamoyo MKOA wa Pwani wametakiwa kutumia fursa waliyoipata na kuwa wajasiriamali Waziri ili waweze kujiajiri na kuwaajiri vijana pakoja na kuwa mabalozi kwa kutoa elimu ya kupiga vita uvuvi haramu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa WILAYA ya Bagamoyo,Mh:Majid Hemed Mwanga wakati mahafali ya wanachuo 21wa wilaya ya Bagamoyo waliokuwa chini ya VETA kwa ufadhili wa benki ya Maendeleo Africa.
Mkurugenzi wa CHUO cha uvuvi Mbegani,Yahya Mgawe amesema uharibifu wa rasilimali za Bahari unatokana na wavuvi kukosa mbinu Za uvuvi pamoja na uhitaji wa samaki soko la kimataifa kuongezeka.
Kaimu Mkurugenzi wa Beta kanda ya Mashariki.Asanterabi Kanza ameishukuru Banki ya Afrika ya Maendeleo kwa kutoa mchango huo kuwawezesha wananchi wa Bagamoyo kupata mafunzo na kuwataka wahitimu hao kuitumia vyema elimu waliyopata kwa maendeleo katika sekta ya uvuvi bagamoyo.
Serikali kwa sasa inasisitiza wananchi wake kufanya ufugaji wa samaki kwa njia ya mabwawa ili kutunza mazingira na kujiongezea kipato.
NGORONGORO LADIES MGUU SAWA MASHINDANO YA SHIMMUTA MOROGORO
-
Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na
program ya...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni