Wanavikundi vya kuweka na kukopa(Vikoba) wa maeneo ya Zingiziwa Chanika wametakiwa kuwakumbuka watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu sanjari na wajane baada ya kupata gawio zao.
Wito huo umetolewa wakati wa kikundi cha MFANO BORA kugawana faida walizojiwekea kwa miaka miwili ya milioni 39 na kuamua kuitoa kwa watu wanye mahitaji maalumu ikiwemo Chakula,mavazi na vifaa kwa watoto wa shule.
Hussein Wambura Togoro ni Diwani wa Kata ya Zingiziwa ambaye ambao anawakumbusha wananchi wengine zaidi kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa ili wanufaike kiuchumi kwa kufuga samaki,Kuku na mifugo mingineyo sambamba na kupata mafunzo ya nidhamu ya fedha.
Naye Mchungaji Alex Erasto Mwanga wa kanisa la KKT chanika ameitaka jamii nchini kuwajali watu wenye mahitaji maalumu na kuwapatia misaada inayostahili kutokana na mazingira magumu waliyokuwa nayo ikiwemo kukosa chakula.
Baadhi ya viongozi wa kikundi cha MFANO BORA wamesema wanajisikia raha kuona binadamu wanaishi kwa Amani na Upendo.
NGORONGORO LADIES MGUU SAWA MASHINDANO YA SHIMMUTA MOROGORO
-
Timu ya mpira wa Netiboli na mpira wa wavu ya Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro imewasili mkoani Morogoro tarehe 25 Novemba 2025, imeendelea na
program ya...
Saa 22 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni