Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, Jana Tarehe 02 Februari, 2017 amemteua Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Venance S. Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.
Jenerali Venance S. Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Major Jenerali James M. Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Major Jenerali James M. Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.
Luteni Jenerali James M. Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Venance S. Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.
Uteuzi huu unaanza mara moja na tarehe ya kuapishwa itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
MBETO: RAIS DKT. MWINYI KUTEKELEZA AHADI ZOTE BILA 'LONGO LONGO' ZANZIBAR
-
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimewatoa hofu waZanzibari kuwa ahadi zote za kisera
zilizoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2...
Saa 16 zilizopita
0 comments:
Chapisha Maoni