Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 03 Juni, 2017 amemteua Bibi Anna Elisha Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Bibi Anna Elisha Mghwira anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Saidi Meck Sadiki aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo.
Wakati huo huo , Mhe. Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo Meja Jenerali Issah Suleiman Nassor alikuwa Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ).
Halikadhalika, Mhe. Rais Magufuli amemteua DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki kuwa Balozi.
Kabla ya uteuzi huo DIGP Abdulrahman Omari Juma Kaniki alikuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi.
Tarehe ya kuapishwa kwa wateule wote itatangazwa baadaye.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
03 Juni, 2017
ASKOFU MWAMALANGA: KILA MTANZANIA ANAWAJIBU WA KUTUNZA AMANI
-
Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya
Madhehebu ya Dini Tanzania, William Mwamalanga, ametoa wito kwa...
Siku 1 iliyopita
0 comments:
Chapisha Maoni