AIRTEL YAGAWA VITABU KWA SHULE YA SEKONDRI YA BWELANYAKE KARAGWE




Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha vitabu vya ada na kiada wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba

Afisa mauzo wa kanda ya ziwa Mohamed Kabeke akikabithi vitabu Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe  bi Siberia Ruboha wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba, akishuhudia ni  Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi
Airtel yagawa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake Karagwe
Airtel Tanzania imeendelea na mradi wake wa kusambaza vitabu katika shule ya Sekondari nchini chini ya mradi wa ‘Shule yetu’ ambapo shule mbalimbali za sekondari nchini zimenufaika na mradi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema kampuni ya Airtel inaendelea kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini hasa tatizo la vitabu vya kiada kwa shule za sekondari.
Kupitia mradi wa ‘Shule yetu’ watoto wengi wa kike watanufaika kwani mradi huu unalenga hasa katika  kumkwamua mtoto wa kike kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi,”

Hawa aliongeza kwa kusema Leo tunatoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake hapa Karagwe Bukoba ikiwa ni mwendelezo wa shughuli zetu za kijamii katika kupambana na tatizo la vitabu mashuleni. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi wa shule ya Bwelanyake kupata nafasi ya kujifunza na kujisomea na kuwawezesha walimu kupata nyenzo muhimu za kufundishia.

Kwa upande wake Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe  bi Siberia Ruboha alisema “elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kushirikiana na Serikali kupunguza tatizo la vitabu vya kiada vya shule za sekondari hapa nchini. Tunaamini msaada huu wa vitabu tulioupata leo utasaidia katika kuinua kiwango cha ufaulu na kuongeza taaluma zaidi kwa wanafunzi wetu na kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi hapa shuleni. /Nachukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wavitumie fursa hii kujisomea na wavitunze vitabu hivi ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi na kutoa matunda bora na mengi zaidi.

Mpaka sasa Airtel kupitia mradi huo imewafikia shule takribani  900 za sekondari nchi nzima kwa kuzipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya  walimu kwa ajili ya kufundishia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List