Wananchi hao wamedai kuwa baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu hasa wakazi wa vijiji hivyo vilivyoguswa na mradi wa Bwawa la maji Kidunda.
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kibulumo Juma Majile amesema wakati wamefika kuelezea mradi wa maji jinsi utakavyokuwa wananchi walikuwa na matumaini makubwa lakini tofauti na hivyo mradi umekuwa kama chanzo cha kutaka kuwaingiza katika janga la Umaskini.
Mkurugenzi Halmashauri ya Morogoro Vijijini Nd,Yona Maki amekiri kupokea malalamiko ya fidia kutoka kwa Wananchi walioguswa na Mradi huo wa Bwawa Kubwa la Maji Kidunda.
Serikali imejipanga kujenga Mradi wa Bwawa kubwa la maji lenye ujazo wa mita milioni 190 litakalo kuwa likitoa huduma katika mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro kwa kusaidiwa na Benki ya Dunia.
Ofisi ya DAWASA
Afisa Habari Msaidizi wa DAWASA aliyejibu majibu ambayo si ya kiungwana kwa Waandishi wa habri
Mkurugenzi Halmashauri ya Morogoro Vijijini Nd,Yona Maki
Ofisi ya mkuu wa wilaya Morogoro.
Ofisi ya mkuu wa wilaya Morogoro.
Wanakijiji wakitawanyika baada ya mkutano kushindwa kutoa majibu ya kufikia muafaka.
Wanakijiji wakitawanyika baada ya mkutano kushindwa kutoa majibu ya kufikia muafaka.
Baadhi ya nyumba za wanakijiji waliopo katika eneo la Mradi
Baadhi ya nyumba za wanakijiji waliopo katika eneo la Mradi
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Kibulumo Juma Majile
Baadhi ya nyumba za wanakijiji waliopo katika eneo la Mradi
0 comments:
Chapisha Maoni