Wazazi wanapofarakana na mtoto kupata malezi ya upande mmoja hali hiyo inasababisha watoto kukosa malezi mema kwa kuwa baadhi ya huduma za muhimu kuzikosa pia wakati mwingine hata mahitaji ya shule bado ni tatizo hali hiyo imechangia watoto kutosoma vizuri,kusoma kwa shida hata baadhi yao kukatisha masomo yao kwa kudanganyika hata kujiingiza kwenye makundi maovu.
Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Temeke Donalds Chavilla amesema ushirikiano wa wazazi ,wanafunzi,Walimu unamanufaa makubwa na kufanya wanafunzi wasome kwa bidii hata kupata wataalam mbalimbali wa kutoka nchini nasio kutegemea kutoka nje,wataalam wa ndani ndio wenyeuwezo mkubwa wa kujenga maendeleo ya taifa.
Afisa Elimu Donalds Chavilla amewataka wamiliki wa shule nchini watumie fursa hiyo kutoa huduma ya Elimu bora nasigeuze ni sehemu ya Kibiashara,zaidi wakifanya hivyo watasababisha kutoa taaruma isiyokuwa bora na kutoa bora elimu,pia amewataka wazazi walipe ada za watoto wao kwa wakati ,na wanafunzi nao wasome kwa bidii kuhitimu kwa kidato cha nne bado awajafika safari yao ya kielimu wanatakiwa kuendelea zaidi kupata elimu ya juu ambayo itaweza kumsaidia mwenyewe kwa miaka ya baadaye.
Afisa Elimu Chavilla ameyasema hayo wakati alipokuwa mgeni rasmi katika MAHAFARI YA 9 ya Kidato cha Nne Pius Sekondary school iliyopo wilaya ya Temeke Kongowe jijini Dar E Salaam jumla ya wanafunzi waliohitimu 128 wavulana .70 na Wasichana 58, wote wametakiwa wasijibweteke kwa hapo walipofikia safari ya elimu bado inawasubili wajitambue kuwa bado ni wanafunzi.
Naye Mkurugenzi wa shule ya Pius Secondary School Mbaulidia .R.Bugingo amewataka wazazi nchini wa walee watoto wao katika misingi iliyo bora ili waweze pata elimu bora na sio bora elimu ,huku akiwasisitiza wanafunzi waliohitimu wasome kwa bidii kwa sababu hamna njia ya mkato katika swala la elimu wajiwekee fikla za kusonga mbele ili wafikie elimu ya Juu
Mkuu wa Shule ya Pius Sekondary school Lucas Hassan amewataka wahitimu hao wa elimu ya kidato cha nne watumie Maadiri mema waliyopata na waendelee nayo pia wasijiamini sana .wanatakiwa wasome kwa bidii pia wamtangulize Mwenyenzi Mungu kwa kila Jambo pamoja na Kusoma kwa bidii,pia akitoa nasaa kuwa shule hiyo inarekodi ya wanafunzi kufahuru ambapo waliohitimu mwaka jana walifahuru wote na kushika nafasi ya kwanza kwa wilaya ya Temeke kwa mkoa wa Dar Esalaam kupata nafasi ya 16 .
Wahitimu wa kidato cha nnePius Sekondary school wakipokea zawadi kwa mgeni rasmi kutokana na kufanya vizuri
Wahitimu wa kidato cha nnePius Sekondary school
Wahitimu wa kidato cha nnePius Sekondary school
Meza kuu siku ya mahafali ya kidato cha nnePius Sekondary school
Wanafunzi wa shule ya Pius Sekondary school
Wazazi wakiwa katika mahafali ya watoto wao Pius Sekondary school
Mkuu wa Shule ya Pius Sekondary school Lucas Hassan
Mkurugenzi wa shule ya Pius Secondary School Mbaulidia .R.Bugingo
Afisa Elimu Donalds Chavilla(Mgeni rasmi siku ya mahafali hayo)
Wanafunzi waliofanya vizuri masomo mbalimbali akipokea zawadi.
Wanafunzi waliofanya vizuri masomo mbalimbali akipokea zawadi.
Wahitimu wa kidato ch nne wakiimba nyimbo za kuwaaga
0 comments:
Chapisha Maoni