Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam DUCE kimefanya Tamasha la kuwakumbusha Walimu nchini kuhusu Vazi la heshima la kuvaa wakiwa Kazini ili waweze kurudisha heshima ya Walimu na kuwa mfano kwa Wanafunzi. Tamasha hilo limefanyika jijini Dar es salaam kuwakumbusha Walimu Mavazi wanayotakiwa kuvaa kutokana na kuwepo kwa baadhi ya Walimu wanaoiga tamaduni za Kigeni kwa kuvaa mavazi ambayo hayana heshima na kuchangia kuporomoka kwa maadili ya Wanafunzi. Katika Tamasha hilo la Vazi la Walimu nchini lilipambwa na Michezo mbalimbali.
Elias Revocatus ni Mwenyekiti wa Kimati ya maandalizi Vazi la Mwalimu amesema Tamasha hilo litasaidia kubadilisha Mavazi ya Walimu.
Waziri wa Sheria wa Wanafunzi Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es salaam DUCE Ezekiel Massangu ameiomba Serikali kuwa na Kampeni za Vazi la Mwalimu katika kila chuo kinachofundisha Kozi za Uwalimu.
0 comments:
Chapisha Maoni